Increase Text Size Decrease Text Size Default Text Size
 
OOPS. Your Flash player is missing or outdated.Click here to update your player so you can see this content.

MEWATA Mail

Username
Password
Uchunguzi wa Matiti - Lindi na Mtwara
Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ITV/Radio one  pamoja na Taasisi ya Wanawake na maendeleo (WAMA) kinapenda kuwatangazia kuwa zoezi la uchunguzi wa saratani ya matiti kwa wanawake sasa  litatolewa katika Mikoa miwili ya Lindi na Mtwara. Zoezi hili litafanyika kwa siku mbili, jumamosi tarehe 8 na jumapili tarehe 9 Mwezi wa Tatu, 2008.

Mkoani Lindi huduma hii ya uchunguzi itafanyika katika Hospitali ya Mkoa ya Sokoine, Hospitali ya Wilaya Nachingwea, Hospitali ya Mission ya Nyangao na Hospitali ya Wilaya Liwale.

Mkoani Mtwara zoezi litaendeshwa katika Hospitali ya Mkoa Ligula, Hospitali ya Wilaya  ya Masasi- Mkomaindo na Hospitali ya Wilaya Tandahimba.

Zoezi Hili litafunguliwa Rasmi na Mheshimiwa Mama Salma Kiwete Jumamosi tarehe 8 mwezi wa Tatu, 2008 mkoani Lindi.

Tunapenda kuwakaribisha wanawake wote wanaoishi mikoa ya Lindi na Mtwara na mikoa ya jirani, kuja kupata huduma hii ya bure ya uchunguzi wa matiti.

MEWATA inatanguliza shukrani zake za dhati kwa wadau wote waliofanikisha mazoezi ya uchunguzi wa saratani ya matiti yaliyopita na tunazidi kuthamini ushirikiano wa wadau wote na wananchi wote kwa ujumla.

Tunaomba ushirikiano wenu katika kufanikisha zoezi hili

Nani kama mama?

 
< Prev   Next >

Polls

Should Breast Cancer Campaigns be extended to cover the whole country?
 

Who's Online

Copyright © 2010 Medical Women Association of Tanzania (MEWATA). All rights reserved.